Rais Dkt. John Pombe Magufuli awaapisha Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amewaapisha mawaziri wane ikulu jijini Dar es Salaam huku wakiahidi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa sera ya hapa kazi tu.

Katika mahojiano na ITV baada ya kula kiapo mbele ya rais Dkt John Magufuli, mawaziri hao wamesema wamejipanga kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali za nchi.
 
Kwa muda mrefu wizara ya maliasili na utalii imekuwa na changamoto kubwa ikiwemo ya kushindwa kusimamia rasilimali asili, lakini huenda suluhisho limepatikana. 
 
Zoezi hilo la uapisho limeshuhudiwa na makamo wa rais na waziri mkuu ambapo mawaziri hao ni pamoja na Prof Jumanne Maghembe ambaye ni waziri wa mali asili na utalii, Dkt Joyce Ndalichako waziri wa elimu sayansi, teknolojia na ufundi, Dkt Philip Mpango waziri wa fedha na mipango, Mhandisi Gerson Lwenge waziri wa maji na umwagiliaji na Prof Makame Mbarawa waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano.            
 







SOURCE:ITV






































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..