Serikali kuwachukulia hatua za kisheria watendaji walioshindwa kudhibiti ujenzi holela.
Serikali imesema haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watendaji walioshindwa kudhibiti ujenzi holela kwenye maeneo ya wazi,taasisi za umma na kuwataka wananchi kuhamisha mali za thamani pamoja na kubomoa majengo yao kwa hiyari kabla hawajavunjiwa kwa kuwa operesheni ya bomoabomoa inaendelea hapa nchini bila kujali uwezo wa mtu.
Tahadhari hiyo imetolewa na naibu waziri,wizara ya ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mh.Angeline Mabulla wakati akizungumza na ITV maeneo ya Buswelu wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza amesema kuwa watendaji wa serikali waliohusika kusababisha migogoro ya ardhi ofisi yake haitawavumilia kwa kuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kuwataka kushiriki kikamilifu katika zoezi linaloendelea la bomoabomoa kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa mwanza bw.magessa mulongo akizungumza katika kikao cha watendaji kilichohusisha madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela amesema kuwa ofisi yake imebaini baadhi ya watendaji idara ya ardhi wanahusika kusababisha migogoro na kuwata wajihuzuru kabla ya kufukuzwa na kushitakiwa.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni