Kasi ya Rais Magufuli ikahamia kwa waziri wa michezo Nape, kafanya maamuzi haya kwa Stand United..



Ikiwa ni siku 13 zimepita toka Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri wa Muungano waTanzania, Dk John Pombe Magufuli atangaze baraza lake la mawaziri, kwa siku 13 tokaNape Nnauye apate dhamana ya kuwa waziri wa michezo, sanaa na utamaduni, amemaliza mgogoro ambao huenda ungeiua Stand United na fedha za udhamini kupotea bila sababu za msingi.
Baada ya headlines nyingi kuandikwa kuhusu mgogoro uliopo ndani ya klabu ya Stand United chama la wana, December 23 waziri wa michezo Sanaa na utamaduni Mheshimiwa Nape Nnauye ametangaza rasmi kumaliza mgororo huo baada ya kumuagiza mkuu wa mkoa wa Shinyanga kuvunja timu ya muda iliyokuwa imeundwa ili kuangalia matumizi ya fedha za udhamini.

“Timu ya Stand United iliomba kuja kuniona waziri wa michezo na kutatua migogoro yao, kwa historia ya hiyo timu imeanzishwa na vijana wa Stand Shinyanga kwa kuchangishana hadi wakapanda daraja, ila baada ya kutokea udhamini wa ACACIA, kukaibuka migogoro kati ya viongozi wa zamani na timu ya muda ya kuwasaidia iliyoundwa na ofisi ya mkuu wa mkoa, wizara imeamua timu ya mkuu wa mkoa ivunjwe na wajiendeshe wenyewe” >>>Nape Nnauye











SOURCE:Millardayo.com























































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..