Nicky Minaj awatumbuiza raia wa Angola
Nicky Minaj awatumbuiza raia wa Angola.
Mwanamuziki wa kufoka wa kizazi kipya kutoka Marekani Nicki Minaj aliwatumbuiza maelfu ya mashabiki katika mji mkuu wa Angola Luanda licha ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati wa kupigania haki za kibinadamu asiandae tamasha hilo la kusherehekea msimu huu wa Krismasi.
Wanaharakati wa The Human Rights Foundation (HRF) walimuandikia barua totoshoo huyo kutoka Marekani wakidai pesa alizolipwa zilitokana na 'faida ya upunjaji wa mali ya umma na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu wanyonge nchini Angola''.
Minaj mwenye umri wa miaka 33 alipuzilia mbali kampeini hiyo na kuandaa shoo ya kukata na shoka Jumamosi usiku.
Shoo hiyo ya kufana iliandaliwa kwa hisani ya kampuni ya simu ya Unitel, ambayo ni mali ya familia ya rais Jose Eduardo dos Santos.
Tangu kukamilika kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe 2002, taifa hilo linalozalisha mafuta mengi zaidi barani Afrika limeshuhudia ukuaji mkubwa wa uchumi kutokana na utajiri wake mkubwa wa madini na mafuta.
Wanaharakati wa The Human Rights Foundation (HRF) wanamtuhumu rais dos Santos kwa kuwahujumu wenyeji kwa kujilimbikizia utajiri yeye na familia yake.
Aidha HRF inasema kuwa Unitel ambayo inamilikiwa kwa kiwango kikubwa na mwanawe rais huyo Isabel dos Santos inatokana na utajiri huo mkubwa usio halali.
Shoo hiyo ya kufana iliandaliwa kwa hisani ya kampuni ya simu ya Unitel
Isabel dos Santos anayedaiwa kuwa ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika aliorodheshwa majuzi katika jedwali la 15 watu wanaoendeleza ufisadi mkubwa zaidi duniani.
Kabla ya kushuka dimbani, Minaj alipiga picha akiwa amejifunika bendera ya ya Angola na nyengine akiwa Isabel dos Santos .
sikujua kuwa ndiye mwanamke wa nane tajiri zaidi duniani.'' aliandika Minaj.
" Lol. Yikes!!!!! GIRL POWER!!!!!
SOURCE:BBC
Maoni
Chapisha Maoni