Wananchi waliojenga nyumba katika eneo la barabara kuu ya Fuoni wavunjiwa nyumba zao...
Wananchi wanaoishi na waliojenga katika eneo linalopita barabara kuu ya Fuoni wameanza kuvunjiwa nyumba zao na maduka huku kukiwa hakuna malipo yeyote ya fidia kutoka serikalini.
Uamuzi huo uemsababisha kero na malalamiko makubwa kutoka kwa wakaazi wa eneo hilo ambapo ITV ilifika katika mtaa huo wa Fuoni na kulikuta Buldoza la kampuni ya MECCO likiendelea na zoezi la kusafisha mtaa huo ili kupanuliwa barabara hiyo ambayo ni moja ya barabara kubwa Zanibar.
Wakiongea na ITV kwa huzuni kubwa wananchi hao wamesema ingawa wanaunga mkono zoezi hilo la serikali lakini ni kwa serikali kukaa kimya huku wao wengine wana hati za nyumba zao kihalali na sio wao waliojenga karibu na barabara ila serikali ndiyo iliyoamua kusogea karibu na nyumba zao.
Juhudi za kuwapata wahusika wa wizara ya miundombinu na mawasilaono hazikufanikiwa kutokana na siku ya jumamosi inagawa taarifa ya wizara iko wazi kuwa wote wanaovunjiwa wamejnga nyumba na maduka kinyume na sheria za baramra huku ujenzi wa barabara hiyi nimuongoni mwa aahdi za serikali wakti wa kampeni.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni