Waziri mkuu aagiza watumishi kwenye halmashauri kuzingatia weledi na uadiliu kazini.
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa amewaagiza watendaji wa halmashauri nchini kutenda kazi kwa uadilifu na kuzingatia maelekezo ya viongozi wa juu ili kuleta tija na kwamba serikali haitamvumilia mtumishi wa umma mzembe, mvivu na asiye muadilifu.
Mh Majaliwa ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani Kigoma, ambapo amesema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kikamilifu na kwa wakati.
Aidha ameagiza kila halmashauri nchini kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwakani wanaanza masomo yao kwa asilimia mia moja ambapo kwa mkoa wa Kigoma amesema serikali itaimarisha ulinzi katika ziwa Tanganyika ili kuondoa uporaji wa zana za uvuvi na ametoa siku mbili kwa mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma ujiji Boniphace Nyambele, Mhandisi na mweka hazina kutoa taarifa kwa katibu tawala mkoa juu ya uuzwaji wa majengo ya maendeleo ya manispaa hiyo Kigodeco yanayolalamikiwa kuuzwa kwa bei ndogo wakati mkuu wa mkoa wa Kigoma akiwa amekataa jengo hilo lisiuzwe.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni