Aliyejifanya Balozi Sefue mbaroni..

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue .Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue . 

Moshi. Polisi mkoani Kilimanjaro, imemtia mbaroni mtuhumiwa wa makosa ya kimtandao, ambaye anadaiwa kutumia jina la Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kutapeli viongozi.
Mbali na kutumia jina la Balozi Sefue, lakini mtuhumiwa huyo alikuwa akisakwa kwa muda mrefu kwa kutumia jina la mwandishi wa gazeti hili mkoa Kilimanjaro, Daniel Mjema kutapeli watu mbalimbali.
Miongoni mwa waliotapeliwa na mtuhumiwa huyo kwa kujifanya ni ‘Daniel Mjema’ ni pamoja na mwenyekiti wa taifa wa Chadema, Freeman Mbowe na wabunge wengine wa CCM na Chadema waliomtumia Sh600,000.
Siku hiyo Novemba 16,2013, mtuhumiwa huyo alimpigia simu Mbowe na kudai ni mwandishi huyo na kwamba amefiwa na mama yake mzazi na maiti ipo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Jijini Dar.
Mbowe aliwahamasisha wabunge wenzake wakiwamo Esther Bulaya wa CCM wakati huo na Grace Kiwelu ambao kila mmoja alichanga rambirambi iliyofikia Sh600,000 na kumtumia mtuhumiwa.
Hata hivyo hakuishia hapo, kwani Januari 16,2014, alimpigia simu Dk Emanuel Nchimbi na kujifanya ni mwandishi wetu huyo na kwamba amefiwa na mkewe na anaomba msaada angalau wa Sh200,000.
Hata hivyo, Dk Nchimbi wakati huo akiwa ni Mbunge wa Songea mjini (CCM), alishtuka na kuupigia simu uongozi wa Mwananchi Communication Ltd (MCL) ambao ulikanusha kuwapo msiba.






SOURCE:Mwananchi




























































































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..