Naibu waziri wa afya Mhe.Kigwangala azuia wafanyakazi waliochelewa kufika wizarani hapo.



Hali ya sintofahamu imewapata wafanyakazi wa wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto mara baada ya naibu waziri wa wizara hiyo Mhe.Dakta Hamisi Kigwangalla kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika ofisi za wizara hiyo kwa kusimama getini kuzuia wafanya kazi wote wa wizara hiyo ambao wamechelewa kufika ofisini baada ya saa 1:30 asubuhi muda ambao ndiyo mwisho wa wafanyakazi kuingia ofisini.

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Mhe kigwangalla amesema kuwa wizara hiyo imekuwa na urasimu mkubwa ambapo wauguzi na madaktari wamekuwa wakilalamika kuwa wizara haitoi huduma ipasavyo ambapo toka amefika wizarani hapo amebaini kuwa wafanyakazi wengi wamekuwa wakitoka na kuingia ofisini wanavyo taka na wengine wamekuwa wakichelewa kufika ofisini. 
 
Ikafika muda wa waziri huyo kutoa maagizo kwa mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa wizara hiyo Bw.Michael John ambapo pia alishauri idara hiyo ufanye mabadiliko ya mfumo wa watumishi kuingia ofisini kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kadi au kidole “BIOMETRIC.
 
Aidha katika hatua nyingine waziri wa wizara hiyo Mhe Ummy Mwalimu hii leo amefanya makabidhiano ya ofisi na aliye kuwa waziri aliyemaliza muda wake Dakta Seif Rashid ambapo Mhe Ummy amepomgeza jitihada mbalimbali alizo zifanya ikiwemo kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuhaidi kutatua baadhi ya changamo walizo zikuta ikiwemo ukosefu wa dawa Mahospitalini.









SOURCE:ITV






















































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..