TP Mazembe Watua Japan Kupigania Ubingwa
Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe wamewasili mjini Osaka, Japan wa michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.
Michuano hiyo itang’oa nanga kesho, Vijana hao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walishinda kombe la klabu bingwa Afrika mwezi uliopita.
Wataanza kampeni yao Osaka Jumapili dhidi ya mshindi wa mechi kati ya Sanfrecce Hiroshima na Auckland City FC ambayo itachezwa Alhamisi.
Mazembe walishangaza ulimwengu miaka mitano iliyopita walipofika fainali ya dimba hilo la dunia lakini wakashindwa na Inter Milan.
SOURCE:Muungwana.com
Maoni
Chapisha Maoni