Tatizo la mgao wa umeme linazidi kuitesa Tanesco Mwanza...



Uongozi wa shirika la ugavi wa umeme Tanzania ( TANESCO ) mkoa wa ,wanza,unadaiwa kumdanganya mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo kwamba kwa hivi sasa hakuna tena tatizo la kukatika kwa umeme katika mikoa iliyounganishwa kwenye Gridi ya taifa,baada ya mashine mbili za gesi za kinyerezi kuanza kufanya kazi.

Wakati tatizo la kukatika kwa umeme katika mikoa ya kanda ya ziwa linalosababishwa na kuzidiwa kwa njia ya msongo wa Kilovoti 220 likiendelea, kaimu meneja wa Tanesco mkoa wa Mwanza Mhandisi Gerson Manase anasema hali ya upatikanaji wa umeme kwa sasa inaridhisha baada ya mashine mbili za gesi za Kinyerezi kuanza kufanya kazi na kuongeza megawati 300 kwenye gridi ya taifa,jambo ambalo limepingwa vikali na mkuu wa mkoa wa Mwanza.
 
Maelezo hayo yamemfanya mkuu wa mkoa huo Magesa Mulongo kuendelea kumbana zaidi kaimu meneja huyo wa Tanesco mkoa wa Mwanza mbele ya wafanyakazi wake.
 
Licha ya shirika la ugavi wa umeme (TANESCO ) mkoa wa Mwanza kukabiliwa na changamoto mbalimbali katika utoaji wa huduma kwa wananchi,ikiwemo ya uchakavu wa miundombinu ya usambazaji umeme, hujuma ya miundombinu ya umeme hasa wizi wa nyaya za shaba na wizi wa vyuma vya nguzo za kusafirishia umeme mkubwa wa 220 kwa kilovoti 132, meneja wa Tanesco kanda ya ziwa mhandisi Amos Maganga anasema mahitaji ya umeme nchini bado ni makubwa.
 
Mkoa wa Mwanza unapokea umeme wa Gridi ya taifa kupitia vituo viwili vya nyakato chenye Transfoma tatu na mabuki kilichopo wilayani Misungwi chenye Transfoma moja.
 





SOURCE:ITV






































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..