Kaya zaidi ya 250 bonde la Mkwajuni hawana makazi ya kuishi kufuatia bomobomoa inayoendelea.



Zaidi ya kaya 250 za bonde la Mkwajuni jijini Dar es Salaam hazina  makazi ya kuishi kutokana na zoezi la bomoabomoa linaloendelea ambapo wameiomba serikali kuwatafuti mahali mbadala pa kuishi kwani hawana njia nyingine mbadala ya kujiondoa katika dhahama hiyo.

ITV ilifika katika eneo hilo na kushuhudia makundi mbalimbali ya wananchi wakiwa hawaamini kinachoendelea kutoka na jinsi tingatinga linavyoshusha nyumba hizo chini huku ulinzi wa jeshi la polisi ukiwa umeimarishwa.
 
Baadhi ya wahanga wa bomoabomoa hiyo wamesema hawana pakwenda na jambo kubwa ni serikali iwatafutiye sehemu nyingine ya kuishi kwani zoezi limekuwa la ghafla sana.
 
Katika kuonyesha kuwa kweli wahanga hao hawana sehemu mbadala ya kwenda baadhi ya watu waliobomoloewa nyumba zao siku ya kwanza bado wanaishi katika eneo hilo pamoja na watoto.
 
Wakizungumzia zoezi hilo afisa mipango miji Dk Charles Mkalawa kutoka wizarani na mwanasheria wa NEMC Bw Mancari Heche Suguta wamesema mpaka sasa ivi zaidi ya nyumba 150 zimebomolewa na zoezi linaendelea.







SOURCE:ITV





















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..