FIFA yawafungia Blatter na Platini kwa miaka minane..
Aliyekuwa Rais wa FIFA Sepp Blatter, katika moja ya mikutano yake huko Russia,Julai 25, 2015.
Rais wa shirikisho la kandanda duniani FIFA, Sepp Blatter aliesimamishwa kazi hivi karibuni alisema mapema Jumatatu kuwa atarudi tena kwenye shirikisho hilo muda mfupi baada ya kamati ya maadili ya soka kumpiga marufuku ya kujihusisha na soka yeye na kiongozi wa shirikisho la soka la ulaya Michel Platini kwa miaka 8.
Kamati hiyo ilichukua hatua hiyo dhidi ya Blatter na Platini kutokana na malipo ya zaidi ya dola milioni mbili ambayo Blatter alimlipa Platini 2011. Hata hivyo waendesha mashitaka wa Uswizi wamefungua mashtaka ya kutaka ufanyike uchunguzi kuhusiana na malipo hayo.
“Blatter alisema hajawahi kudanganya kuhusu fedha” akieleza kuwa alifanya mawasiliano ya maneno na Platini kwa ajili ya dola milioni mbili. “Ninajijutia namna kamati hii inavyofanya. Kamati hii haina haki ya kufanya hivyo dhidi ya rais”.
Majaji wa FIFA walisema ushahidi juu ya mawasiliano hayo “haukuridhisha na ulikataliwa”. Akizungumza mjini Zurich,. Blatter alijieleza yeye ni mtu mwenye maadili. Alisema kanuni zake mbili ni kutotumia fedha ambazo hajazifanyia kazi na kulipia madeni.
Michel Platini
Marufuku hiyo inaonekana itaathiri juhudi za Platini kuchukua nafasi ya Blatter kwenye uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi wa Februari. Viongozi hao wote wawili ambao wanakanusha kufanya jambo lolote wanatarajiwa kukata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya FIFA na mahakama inayohusika katika masuala hayo ya michezo.
Blatter na Platini wote awali walipigwa marufuku tangu mwezi Oktoba kutokana na utata juu ya malipo ya fedha.
Shirikisho la kandanda duniani-FIFA
FIFA iliingia kwenye kashfa ya rushwa baada ya maafisa 14 wa FIFA walipokamatwa mjini Zurich mwezi Mei na kufunguliwa mashtaka na Marekani kwa takribani makosa 50 ya rushwa ikiwemo wizi wa fedha kwa kutumia akaunti batili. Maafisa wa uswisi pia wamefungua mashtaka tofauti ya uchunguzi wa uhalifu unaohusiana na chaguo la FIFA kwa nchi ya Russia na Qatar kuwa wenyeji wa matamasha ya michezo ya kombe la dunia mwaka 2018 na mwaka 2022 bila kufuata kanuni.
SOURCE:VOA
Maoni
Chapisha Maoni