Kamati ya halmashauri kuu ya CCM Zanzibar yakutana kujadili hali ya kisiasa Zanzibar.



Siku moja tu baada ya rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein kukutana na rais John Pombe Magufuli, kamati maalum ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM Zanzibar imekutana kujadili hali ya kisiasa Zanzibar.

Akitoa taarifa za kikao hicho katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Zanzibar Waride Bakari amesema kikao hicho kimeunga mkono mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa Zanzibar ambapo mazungumzo hayo yanahusisha viongozi wa juu wa serikali hata hivyo imewataka wana CCM kujiandaa na marudio ya uchaguzi kwa vile uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi.
 
Aidha kiongozi huyo wa CCM amesema hata kama muda wa miezi mitatu itapita na kutopatikana ufumbuzi wamgogoro huo na tume kutotoa tarehe mpya ya uchaguzi rais wa Zanzibar Dr Ali Mohmaed Shein kwa mujibu wa katiba ataendelea kuwepo madarakani hadi hapo rais wa awamu mpya atapochaguliwa na kuapishawa.
 
Wakati CCM na CUF wakiendelea na mazungumzo yao chama cha ADA -TADEA kupitia kwa mkurugenzi wake wa habari na ufundi Rashid Mchenga kimesisitiza umuhimu wa kufuatwa kwa katiba na sheria huku kikishangazwa kuona ni vyama hivyo tu vianvyojadilaina wakati uchaguzi huo ulikuwa na wagombea 14.
 
Ni miezi miwili sasa tokea kufutwa kwa uchgauzi mkuu wa Zanzibar huku tume ya uchaguzi hadi leo haijatoa taarifa yeyote kuhusu uchaguzi huo na wananchi wazanzibar wanaendelea na harakati zao kama kawaida.






SOURCE:ITV



























































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..