Kampuni Ya Magari Ya Volkswagen Inatarajia Kuonesha Magari Yanayotumia Umeme Wakati Google Na Ford Magari Yanayojiendesha Yenyewe..
Kampuni ya magari aina ya Volkswagen inatarajia kuyaonesha magari yao yanayotumia umeme ama magari ya kuchaji, wakati kampuni ya GOOGLE na FORD pia ni kampuni za magari zeneyewe zinalingana kwa kutengeneza magari yanayo tembea yenyewe bila dereve.
Magari hayo yatakuwa ni sehemu kubwa ya wateja wao wanaopendelea kutumia magari ya aina hiyo nchini marekani na dunia kwa ujumla. Na Kampuni ya Volkswagen na Ford tayari wenyewe walikuwa wamesha toa taarifa juu ya ujio huo wa magari yao kabla hata ya kuyaonesha hadharani ambayo watayaonesha mapema mwakani mwezi wa kwanza.
Google na Ford wenyewe wataungana kwa pamoja kuunda umoja wao katika kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe.
Kampuni ya FORD wamesema mapema mwezi huu wanampango wa kuyajaribu magari hayo yanayojiendesha yenyewe bila dereva katika mitaa ya California wakati GOOGLE wenyewe tayari walisha yajaribu barabarani katika miji ya California na Texas Marekani.
SOURCE:Forbes
Maoni
Chapisha Maoni