Baadhi ya wakazi wanadaiwa kuvuna miti kwenye msitu wa hifadhi kinyume na sheria Muheza..
Baadhi ya wakazi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya kijiji cha Kwamsoso kilichopo kata ya Misalai wilayani Muheza, wanadaiwa kuvuna miti aina ya mivule zaidi ya heka 5 iliyopo katika msitu wa hifadhi ya asili wakidai kuwa wameomba kwa mamlaka husika ngazi ya wilaya hiyo kuwa wanataka miti mitatu kwa ajili ya ujenzi wa maabara na zahanati.
ITV imeshuhudia uharibifu huo wa misitu ambapo wajumbe wa kamati za misitu za kijiji cha Kwamsoso ambao hawakushirikishwa katika zoezi hilo wamesusia kundelea na kazi ya kudhibiti uharibifu huo kufuatia kitendo cha uvunaji haramu wa misitu yenye vijito vya maji yanayotumika wilayani Muheza na jijini Tanga kuharibiwa vibaya.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Misalai Bwana Bughe George akifafanua zaidi kuhusu mbinu walizotumia viongozi wa serikali kuwahujumu wajume wa kamati maalum iliyoundwa na mkuu wa wilaya kuhusu tatizo hilo amesema walipofika katika eneo la msitu huo waliwapeleka katika eneo lingine kisha kuridhika na kuwasilisha taarifa kwa mkuu wa wilaya kuwa hakuna uharibifu.
Kufuatia hatua jitihaza za kumpata mkuu wa wilaya ya Muheza kuelezea sakata hilo bado zinaendelea huku baadhi ya wajumbe wa kamati ya kuhifadhi msitu huo wameazimia kuachana na zoezi la kulinda msitu wa hifadhi wakidai kuwa viongozi wao wa serikali ya kijiji cha kwamsoso wameshindwa kujenga uaminifu katika zoezi hilo.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni