Zaidi ya abiria 300 na watoto 67 wamenusurika kufa baada ya bot ya Roy kuungua moto Unguja.
Zaidi ya abiria 300 na watoto 67 waliokuwa wakisafiri na bot ya Roy wamenusurika kufa baada ya boti hio kuungua moto na baadae kuzima kabisa na kuelea baharini ilipo kuwa ikitokea Unguja kwenda Kisiwani Pemba majira ya saa 3.30 asubuhi hivi leo.
Kwa mujibu wa abiria walokuwemo kwenye boti hio ya Roy iliokuwa ikitokea Unguja kuja Bandarini mkoan Kisiwan Pemba amesema walishuhudi moshi nzito ukitokea ndani ya chumba cha ingen chini ghafla safari yao ilisimama kwa boti kuzima moto na kuelea hadi walipookolewa na Serengeti ilio kuwa ekienda Unguja kwa kukatisha safari kufungasha kuileta hadi bandarini.
Capten wa boti hio Mohamed Ali Khamis amewambia viongozi wa serikali walio fika katika tukio hilo kuwa wakiwa karibu kufika kisiwani Pemba boti yao imepasuka mpira wa paipu ya haydrolic ya mafuta ndio ilio sababisha kuwaka moto hata hivyo hakuna mashine ilio ungua kwavile waliwahi kuuzima moto huo kwa mashirikiano na Mv Serengeti nakufika bandarini salama.
Mkuuu wa mkoa Kusini Pemba Bi Mwanajuma Majidi Abdalla aliefika katika tukio hilo kujionea eneo liliungua ndani ya boti amewataka wamiliki wa vyombo vya kusafiria baharini nchi kavu na angani kuvifanyia matengenezo ya mara kwa mara nae kamanda wa polisi mkoa kusini Pemba kamishina msaidizi Mohamed Shekhani Mohamed amethibitisha kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa abiria wawili wame lazwa Abdalla Mzee baada ya kupata mshituko.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni