Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yakabidhiwa rasmi meli ya MV Mapinduzi II.
Siku moja tu baada ya kuzinduliwa kwa meli ya mapinduzi 2 na rais wa Zanzibar, kampuni iliyojenga meli hiyo ya Daweoo ya Korea Kusini imekabidhi rasmi meli hiyo kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Makabidhiano hayo yamefanyika hapa Zanzibar ambapo seriklai ya mapinduzi ya Zanzibar iliwakilishwa na katibu mkuu wa wizara ya fedha Khamis Mussa ambaye alisaini kwa niaba ya SMZ wakati Kim Yeon -Woong ambaye ni mkurugenzi wa mindombinu wa tassi hiyo alisaini kwa niaba yao.
Akizungumza baada ya makabidhiano hayo katibu mkuu Khmais Mussa amesema seriklai imeridhika na ujenzi wa meli hiyo kwa vile mambo ya msingi waliyokubalaina nayo yametekelezwa na wanatarajiwa kumaliza malipo ya mwisho wakati wowote kuanzia sasa.
Naye katibu mkuu wa wizara ya miondomniu na mawasialono wazanzibar Dr Juma Malik Akili amesema utaratibu wa kisheria utatumuka katika ununuzi wa meli hiyo na hakuna udanganyifu wa aina yeyote uliofanyika kuhusu ununuzi wa meli hiyo kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Meli hiyo ya mapinduzi 2 iliwasili wiki iliyopita na imejengwa na kununuliwa na serikali kwa dola za marekani milioni 30 meli hiyo inatarajiwa kuanza kutoa huduma ya usafiri wa uhakika katika bandari za Pemba, Unguja na Dar es Salaam.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni