Waziri Muhongo akerwa na mhandisi wa maji...
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
Profesa Muhongo alitoa agizo hilo juzi alipokuwa katika kikao cha wadau wa maendeleo Musoma vijijini mkoani Mara kwa lengo la kupambana na umaskini, ujinga na njaa.
Muhongo alimwagiza Mkurugenzi huyo kumshusha cheo mhandisi huyo kwa kile alichodai kuwa ameonesha dhahiri hawezi kwenda sambamba na utendaji kazi wa kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu.
“Mkurugenzi nitafuatilia kujua kama huyu mhandisi umemshusha cheo, watu kama hawa wanaturudisha nyuma, hawatembelei miradi wanakaa ofisini na kusubiri taarifa, ndiyo maana hajui hata jina la kijiji kimoja,”alisema Muhongo na kuongeza:
“Mchukue wa chini yake apande cheo na huyu mshushe cheo kuanzia kesho, sitaki kusikia tena lolote kutoka kwake, atasababisha jimbo langu likwame katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Myovela alimweleza Waziri kuwa agizo hilo amelipokea na atalifanyia kazi, huku akifafanua mradi huo kwa kusema kuwa mradi huo upo kwenye tathimini kwa vijiji zaidi ya 10 na utakamilika kwa zaidi ya kipindi cha miaka mitatu.
Maoni
Chapisha Maoni