Watu Millioni 15 kupiga kura Uganda.

Vijana wa Uganda wanamsubiri Papa kuwasili Kolo kuwahutubia.
Vijana wa Uganda wanamsubiri Papa kuwasili Kolo kuwahutubia.


Tume ya uchaguzi ya Uganda imetoa idadi kamili ya wapiga kura nchini humo ambayo ni wapiga kura 15,277,196. Idadi hiyo pia imetolewa katika orodha ya raia wa Uganda waliosajiliwa kupata vitambulisho vya kitaifa.
Wapiga kura nchini Uganda hata hivyo watashiriki uchaguzi bila kadi za kupigia kura, na si sharti mpiga kura awe na kitambulisho cha kitaifa. Uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika Februari 2016 na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Dr. Baduchi Gundu ameomba watu wote “kuendelea kushiriki nasi katika safari hii ya uchaguzi”.
Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo haikundaa zoezi la kuwasajili wapiga kura    kama sehemu ya matayarisho ya kuandaa uchaguzi mkuu .
Shughuli iliyoandaliwa na wizara ya mambo ya ndani ya kuwapatia wananchi vitambulisho vya uraia ilihusisha hata wale walio na umri wa miaka 16 ilitoa fursa nzuri ya kupata majina ya wapiga kura.
Lakini wakifafanua kwamba wale tu walio na umri wa miaka 18 au zaidi ndio watakaoruhusiwa kupiga kura .
Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imefafanua kwamba orodha ya wapiga kura ndio itakayotumika na si orodha ya raia waliopata vitambulisho, lakini wamepewa ombi kwamba kama wakiwa na vitambulisho wanaweza kuchukua ili kurahishisha kazi ya  wasimamizi wa uchaguzi.









SOURCE:VOA









































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..