Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2016

Good News kwa muziki wa Afrika Chris Brown kampa dili Wizkid..

Picha
Najua jina la  Chris Brown  sio geni masikioni mwa watu wanaopenda muziki, basi leo May 29 2016 huenda ikawa ni good news kwa muziki wa Afrika, baada ya msanii kutoka Marekani  Chris Brown  kumpost msanii  Wizkid   kutoka  Nigeria . Katika ukurasa wake wa Instagram  Chris Brown  amempost  Wizkid  na kuandika maneno machache sana, lakini yanatafsirika kama kumualika mkali huyo wa  Nigeria  katika tour yake ya  One Hell Of Nite Tour  kwa mwaka 2016 atakayoifanya bara la Ulaya katika nchi za  Uholanzi ,  Ujerumani  na  Denmark . Muda mchache baada ya  Chris Brown  kupost picha ya  Wizkid , staa huyo kutokea Nigeria  alipost nae picha kama hiyo na kuthibitisha kuwa kuanzia June 5 hadi June 11 2016 atakuwa katika  #OneHellOfANiteTour   pamoja na  Chris Brown . Source:Millardayo.com ...

PICHA YA SIKU NA TASWIRA BLOG

Picha

Daktari asimamishwa kazi kwa uzembe uliosababisha kifo Mkoani Mara.

Picha
Uongozi wa halmashauri wa wilaya ya Butiama  mkoani Mara umemsimamisha kazi daktari  mwandamizi  wa hospitali  wa Wilaya hiyo na kutoa  onyo kali kwa mtaalam  mmoja  wa maabara  baada ya kudaiwa kufanya kazi kwa uzembe hatua ambayo imesababisha kifo cha mtoto Stephen Julius mwenye umri wa miaka minne mkazi wa kijiji cha Butiama.  Kusimamishwa kwa daktari huyo Dk Henri Japhat Msusa kunafuatia tume iliyoundwa  na uongozi wa hospitali hiyo muda  mfupi tu baada ya    mtoto huyo afariki dunia na maelezo ya uzuni na kina ambayo yametolewa na mama mzazi wa mtoto huyo Bi.Pilly Juma James, mbele ya mkuu wa mkoa wa  Mara Bw Magesa Mulongo katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika kijijini Butiama.     Akitoa taarifa ya uchunguzi wa tume iliyoundwa na uongozi wa hospitali hiyo ya Butiama na sababu ambazo zimesababisha kifo cha mtoto huyo,Mganga Mkuu wa halmashauri ya Butiama Dk Archard Rwezahura,  ...

Tamko la Waziri Makamba kuhusu siku ya mazingira duniani..

Picha
TAMKO LA MHE. JANUARY Y. MAKAMBA (MB), WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) KUHUSU SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI TAREHE 29 MEI, 2016 Ndugu Wananchi; Tarehe 5 Juni, 2016 Watanzania tutaungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Mazingia Duniani. Kama mnavyofahamu   Baraza la Umoja wa Mataifa la mwaka 1972, wakati wa mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa uliohusu Mazingira huko Stockholm, nchini Sweden liliamua kuwa tarehe 5 Juni ya kila mwaka iwe ni Siku ya Mazingira Duniani. Aidha, Azimio la kuunda Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Mazingira Duniani, yaani  United Nations Environment Programme (UNEP) , lilipitishwa siku hiyo. Tangu wakati huo, nchi mbalimbali duniani zimekuwa zikiadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kila mwaka tarehe 5 Juni, kwa ujumbe maalumu unaotolewa na Umoja wa Mataifa. Ndugu Wananchi; Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kutoa fursa kwa jamii duniani kutambua na kuwa na ...

Kenya yasisitiza kuzifunga kambi za wakimbizi..

Picha
Kenyatta Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa hatobadili uamuzi wake wa kuifunga kambu kuu ya Dadaab,makao ya zaidi ya raia 300,000 wa Somalia. Taarifa kutoka afisini mwake inasema kuwa amemuambia naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson kwamba hatua hiyo haitabadilishwa. ''Treni imeondoka kituoni .Kwa hivyo ni wale wanaotaka kuona ufanisi wa safari hiyo wangie ndani'',aliongezea. Makundi ya msaada na shirika la wakimbizi katika Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea wasiwasi wake kuhusu kufungwa huko. Bw Kenyatta amesema kuwa kufungwa kwa kambi hizo kutashughulikiwa kwa njia inayofaa.Matamshi yake yanajiri siku moja tu baada ya rais wa Somalia Kuonya kuusu kufungwa kwa kambi hiyo. Source:BBC

Kitwanga azidi ‘kupigwa za uso’

Picha
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga. Siku moja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga kutimuliwa nafasi hiyo kwa ulevi, wabunge na wasomi wameendelea kumbana zaidi wakisema hatua hiyo ya Rais imechelewa. Wapinzani wamekuwa wakimtaka Rais amuondoe kwenye nafasi hiyo kutokana na kuhusishwa na Kampuni ya Infosys ambayo ilitoa ushauri kwa Kampuni ya Lugumi Enterprises iliyopewa zabuni ya kufunga vifaa vya kuchukua alama za vidole (AFIS) katika vituo vya polisi. Wakati wasomi wakisema hayo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi huo ulikuwa sahihi na swali ambalo Kitwanga hakulijibu vizuri kutokana na hali ya ulevi, litapaswa kujibiwa upya baada ya wabunge kuomba mwongozo wa swali hilo. Majaliwa alisema Rais ametengua uteuzi wa Kitwanga kuanzia juzi baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. “Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake...,” alisema Majaliwa. Alisema uamuzi wa Rais Magufuli umefu...