Sukari yapanda bei hadi 4000 kwa kilo..
Licha ya Rais John Magufuli kuwataka wafanyabiashara kutokuficha sukari na kupunguza bei yake, hali inaendelea kuwa tofauti katika jiji la Mwanza na vitongoji vyake ambapo bei ya bidhaa hiyo kwa kilo jana imefikia Sh4, 000.
Katika kata za Igogo, Pamba, Mahina, Mbugfani, Mabatini, Mkuyuni, Nyegezi, Butimba kilo moja jana iliuzwa Sh4, 000 huku baadhi ya maduka ya rejareja yakisitisha kutoa huduma hiyo.
Kutokana na hali hiyo, wananchi wameiomba serikali kuchukua hatua madhubuti ili kunusuru hali hiyo kwani kila kukicha mambo yanazidi kubadilika hivyo kuwaongezea ugumu wa maisha.
Bei ya jumla katikati ya jiji la Mwanza na kata ya Kisesa wilayani Magu mfuko wa kilo 50 unauzwa kwa Sh180, 000.
Wakizungumza na mwananachi baadhi ya wananchi walisema serikali haina budi kuruhusu sukari kutoka nje ya nchi ili kuwanusuru na ugumu wanaoupata kwani wengi wameshindwa kumudu bei hiyo na kuwasabishia adha.
“Hii ina inaleta picha gani? kila rais anaposema kupunguza bei ya bidhaa hiyo na kuifichua sukari iliyofichwa kwenye maghala, ndipo bei huzidi kupanda mara dufu, jana (juzi) kilo moja ilikuwa inauzwa Sh3500 lakini leo(jana) imepanda zaidi kufikia 4000,” amesema Juma Masanja mkazi wa Bugarika.
Baadhi ya wauza maduka wa rejareja walisema wameacha kuuza bidhaa hiyo kutokana na kupanda zaidi bei yake na kushindwa kumudu.
“Kwasasa tangu bei ipande hata biashara hii imekuwa ya shida, wananchi wengi wanalalamika kupanda kwa bei, wengi hawanunui hata sisi tumeacha kwani ukiileta ni hasara itakaa ndani wakati mtaji wenyewe ni kidogo” amesema Irene Kapaya mkazi wa kata ya Nyegezi.
Maoni
Chapisha Maoni