Lema ashauri kufungwa vifaa maalumu ndani ya bunge vya kupima ulevi na kupongeza maamuzi ya Rais Kumfuta Kazi Kitwanga..

 
Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mh. Godbles Lema ameshauri kufungwa kwa vifaa maalum vinavyopima ulevi ndani ya bunge  ilikulinda heshima ya Muhimili huo wa bunge.

Katika mahojiano Maalum na ITV Dar es Salaam waziri huyo kivuli pamoja na mambo mengine amepongeza uamuzi wa rais wa kumfuta kazi aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani ya nje Charles Kitwanga huku akisema ni dhahiri kiongozi huyo amechafua hadhi ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi.
 
Katika Mahojiano hayo Lema amekiri kitendo cha unywaji wa Pombe kupitiliza kwa kiongozi ni utovu wa nidhamu jambo ambalo huenda likazidi kushusha hadhi ya bunge ambalo ni Mahususi kwa kutunga sheria na kuisimamia Serikali.
 
Haya yanakuja ikiwa ni siku moja tu baada ya taarifa ya Ikulu ya Dar es Salaam kutangaza kumtimua kazi aliyekuwa waziri wa mambo ay nadni ya nchi baada ya kuingia bungeni na kujibu swali la wizara yake kimakosa huku akiwa amelewa.




Source:ITV



































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..