Wajibu wa Vyombo vya habari Barani Afrika ni kuwa na uzalendo wa kupenda, kulinda na kutetea maslahi ya nchi zao.


Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr. Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akitoa Mhadhara katika Chuo cha Ulinzi Cha Taifa Kunduchi jijini Dar es salaam, kuhusu Wajibu wa Vyombo vya Habari binafsi katika ulinzi wa Taifa.

Amesema viongozi wa serikali kwa kupitia vyombo vyake vinahitajika kuweka utaratibu wa kukutana mara kwa mara na waandishi wa habari waandamizi ili kuwafafanulia mambo mbalimbali yanayohusu mustakabali wa taifa ili kuvipa uwezo vyombo vya habari kutekeleza uzalendo wao kwa nchi zao kupitia habari wanazoziandika na kutangaza.
 
Akijibu swali kuhusu uwezekana wa nchi kutekwa nyara na kundi la watu wachache wenye maslahi binafsi, hususan wakati wa uchaguzi mkuu, Dr. Mengi amesema jambo hilo linatokea penye rushwa iliyokithiri, na kusisitiza kuwa dawa yake ni kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa.
 
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa Meja Jenerali Yacoub Mohamed amesema chuo hicho kilichoanzishwa mwaka 2012 hutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi  kwa viongozi waandamizi wa umma na sekta binafsi kutoka nchini na nje ya nchi:..

Mkuu huyo wa Chuo amesema sasa hivi chuo kinaendesha awamu ya nne ya mafunzo kwa kuwashirikisha wanachuo 38, wakiwemo Watanzania 26 na wengine 12 wanatoka  nchi za Burundi, Uganda, Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Botswana, Namibia, Nigeria, Malawi na China, lengo likiwa kutoa mafunzo kwa viongozi waandamizi wa serikali na sekta binafsi.




Source:ITV






































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..