Wabunge wajadili bajeti ya kwanza ya Magufuli..
Rais Dkt.John Pombe Magufuli.
Wabunge wa tanzania wanakutana katika mji mkuu wa Dodoma kujadili na kuidhinisha pendekezo la bajeti ya utawala wa rais John Magufuli kwa mwaka huu, kwa mujibu wa waziri wa habari Nnape Nnauye.
Bunge linapanga kukamilisha utaratibu wa kuidhinisha bajeti mwezi Julai. Itakuwa ni bajeti ya kwanza ya Magufuli tangu ashinde uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.
Asilimia 40 ya mapendekezo ya bajeti itakuwa ni maendeleo ya miradi ya kitaifa, ikiwa ni mabadiliko makubwa kutoka utaratibu wa awali ambapo bajeti ya maendeleo ilikuwa katika kiwango cha asilimia 27 anasema Nnauye.
“Kwasababu ni bajeti yake ya kwanza, watu nchini Tanzania wanatarajia mengi zaidi….Tumezungumzia kuhusu mchakato wa viwanda Tanzania. Watanzania wanatarajia kwamba bajeti hii itafufua utaratibu wa viwanda nchini, kuongeza ukuaji wa uchumi, itafungua fursa za ajira na inatarajiwa kuboresha viwango vya hali ya maisha kwa watu wengi humu nchini,” amesema Nnauye.
Matarajio miongoni mwa watanzania ni makubwa kwasababu ya hatua za Magufuli ambazo amechukua tangu aapishwe kushika madaraka. Hii ni pamoja na ziara za kushtukizaz kwenye taasisi za serikali, ambazo serikali inasema zimelenga kuhakikisha uwajibikaji na kuboresha maadili ya kazi miongoni mwa wafanyakazi katika sekta za umma.
Rais Magufuli pia ametoa amri ya kupiga marufuku ziara za maafisa wa serikali nje ya nchi ambazo zinagharimi fedha nyingi za walipa kodi.
Maoni
Chapisha Maoni