Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani aridhishwa na uwezo wa kijeshi wa Tanzania.
Majenerali na wakuu wa majeshi ya nchi kavu kutoka nchi za bara la Afrika walikutana Arusha kujadili changamoto za kiusalama katika nchi za Afrika wameshudia mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa na jeshi la nchi kavu la Tanzania yaliyofanyika katika eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli.
Miongoni mwa makamanda walioshuhudia mazoezi hayo ni Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani Jenerali Mark Milley na makamanda wengine ambao kwa muda wote walionyesha kushangazwa na uwezo mkubwa wa matumizi ya dhana za kisasa walionao askari wa Tanzania.
Wakizungumzia baada ya mazoezi hayo baadhi ya makamanda wa Jeshi la Tanzania waliwaeleza majenerali hao kuwa mafanikio na uwezo wa Jeshi la Tanzania ambalo limekuwa likisaidia nchi mbalimbali za Afrika ni nidhamu na umakini wa namna ya kuwapata vijana wenye sifa ya kuwa wanajeshi.
Majenerali na Makamanda wakuu wa majeshi ya nchi kavu kutoka nchi za Afrika wanatarajiwa kutoa mapendekezo yao ya nanma ya kudumisha usalama katika nchi za Afrika hapo kesho.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni