Messi ampa somo Aguero kuhusu Pep Guardiola..
Baada ya Pep Guardiola kuteuliwa kuifundisha timu ya Manchester City kwa msimu ujao, Aguero amefunguka kuhusu somo alilopewa na Messi kuhusu kocha huyo.
Timu ya Manchester City imeonekana kushindwa kufanya vizuri msimu huu kwenye ligi kuu ya Uingereza japo imefanikiwa kufika kwenye hatua ya nusu fainali za Uefa kwa mara ya kwanza mwaka huu. Aguero alisema wana matumaini kuwa Pep Guardiola ataizoea klabu na kuamua namna gani wanatakiwa kucheza lakini ni jambo la msingi kupiga hatua kubwa zaidi msimu ujao.
“Leo [Messi] ameniambia ni mtu mzuri sana, na wachezaji kadhaa niliozungumza nao wamesema hivyo pia. Simjui kwa undani lakini tutaona baada ya Copa America [nikiwa na Argentina] nini kitatokea. Nitamfahamu vizuri na atatusaidia sote,” ameongeza.
Aidha Aguero amesema kuwa walijua kuwa wanayo timu bora lakini haikuwa imara kushinda ligi ya mabingwa.
Source:BONGO 5
Maoni
Chapisha Maoni