Justin Bieber: Sitapiga picha na mashabiki..


Justin Bieber asema hatopiga picha tena na mashabiki wake
Iwapo hujagundua basi ujue kwamba nyota wa muziki wa Pop Justin Bieber yuko katika ziara ya ulimwengu.
Kwa sasa yuko nchini Marekani ambapo alionekana amepumzika katika mbuga moja kabla ya tamasha yake mjini Boston.
Image captionBieber alivyoandika katika mtandao wa instagram
Bieber ambaye alikuwa hana viatu aliwavutia mashabiki lakini akakataa kuzungumza nao hadi watakapoweka simu zao chini.
Haijulikani iwapo picha alizochukua na mashabiki wake katika lango la mbuga hiyo zilikuwa za mwisho,lakini baadaye jioni alichapisha katika mtandao wake wa Instagram kwamba hatapiga picha tena na mashabiki.



Hivi ndivyo mashabiki wake walivyomjibu

''Iwapo utakutana nami mahali ujue kwamba sitapiga picha tena'',aliandika.
Alielezea vile watu hawaezi hata kumsalimia ama kujua kwamba hata yeye ni binaadamu na hivyobasi kumfanya kujihisi kama mnyama na sasa anataka kuheshimiwa.
Justin Bieber aiwa nchini Marekani


Aliongezea: Najua kwamba watu hawatafurahia lakini hakuna mtu anayenidai picha.




Source:BBC




































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..