MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA NA KUMZIKA MAREHEMU PAPA WEMBA...
Mwanamuziki Papa Wemba aliyefariki wiki iliyopita nchini Ivory Coast amefanyiwa ibada ya mazishi katika kanisa la kanisa kuu la Notre Dame Kinshasa ili kuweza kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele leo.
Ibada hiyo imefanyika baada ya wananchi kupewa fursa ya kuuaga mwili wa nguli huyo wa muziki kwa muda wa siku tatu baada ya kufikishwa nchini humo kutokea Ivory Coast.
Gwiji huyo wa muziki wa lingala alizaliwa mnamo Juni 14 mwaka 1949, katika eneo la Lubefu, Wilaya ya Sankuru nchini DR Congo.
Baadhi ya nyimbo zake ambazo ziliwika sana ni pamoja na Mwasi, Show me the way, Yolele, Mama, P na Rail On.
Aidha Papa Wemba alifariki baada ya kuzirai wakati akiendelea na tamasha mjini Abidjan Ivory Coast April 24 2016.
Source:Lindiyetu.com
Maoni
Chapisha Maoni