Wabunge: Kwa nini miradi ya mwaka jana itengewe fedha mwaka huu?
Kamati ya Bunge imehoji miradi iliyowahi kutengewa fedha katika awamu iliyopita ya bajeti inayopita, iweje itengewe fedha katika bajeti inayojadiliwa hivi sasa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Mary Nagu amehoji leo kwa niaba ya kamati yake alipokuwa akiwasilisha maoni yao kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/17.
Amesema uchambuzi uliofanywa na kamati hiyo umebaini miradi mbalimbali ya maendeleo inayotengewa fedha kwa mwaka 2016/2017 ni mwendelezo wa utekelezaji wa ile ya mwaka unaomalizika wa fedha pamoja na miradi mipya ya 2016/17.
“Mwenendo huu unalifanya Bunge lijadili bajeti mpya kwa ajili ya miradi mipya ya maendeleo wakati kiuhalisia ni bajeti ya miradi ileile ya zamani,”amesema.
Kamati hiyo ililiomba Bunge liitake Serikali kukamilisha miradi iliyopo kabla ya kuanzisha mipya.
Maoni
Chapisha Maoni