Serikali yaagiza Ofisi ya CAG kutoa majibu ya ufujaji fedha zaidi ya Milioni 773.5,Bahi na Chamwino...
Serikali imeiagiza ofisi ya Mkaguzi na mdhibiti wa mahesabu ya Serikali –CAG kufanya ukaguzi na kutoa majibu haraka iwezekanavyo kuhusiana na ufujaji wa fedha zaidi ya shilingi milioni 773.5 katika miradi mitatu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi katika wilaya za bahi na chamwino mkoani dodoma.
Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Luhaga Mpina ametoa agizo hilo baada ya kuikagua miradi hiyo ambayo inahusiana na umwagiliaji pamoja na upatikanaji wa nishati jua na kubaini kuwa ipo chini ya kiwango na kwamba haikidhi matakwa ya wakazi wa wilaya hizo.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni