Migiro ateuliwa balozi wa Uingereza..
Dk Asha Rose Migiro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amemteua Dk Asha Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Dk Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Kabla ya wadhifa huu, Dk Migiro alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba kwenye serikali ya awamu ya nne.
Dk Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho, katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Maoni
Chapisha Maoni