Simba waliotekwa Peru watua Afrika Kusini..
Simba waliotekwa Peru watua Afrika Kusini
Simba 30 waliookolewa nchini Peru na Colombia wamewasili nchini Afrika Kusini baada ya kusafirishwa kwa ndege na shirika la kupigania haki za wanyama.
Waandishi wa habari walisema kuwa simba hao walionekana wenye afya licha ya kuchoka kufuatia safari ndefu kutoka Amerika ya Kusini.
- Simba hao waliolelewa kizuizini waliokolewa na wapiganiaji wa haki za wanyama wa kimataifa Animal Defenders.
Kundi hilo ambalo walipigania kubadilishwa kwa sheria na kuharamisha wanyama kutumiwa katika utumbuizaji na sarakasi.
Simba hao watapelekwa eneo moja la kuwatunza Kaskazini mwa Afrika Kusini ambapo wataishi maisha yao yote.
Simba hao watapelekwa eneo moja la kuwatunza Kaskazini mwa Afrika Kusini
Badhi yao meno na makucha yao yameng'olewa na itakuwa vigumu wao kuishi mbugani.
Source:BBC
Maoni
Chapisha Maoni