Bunge lapitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya rais Tamisemi shilingi trilioni 6.02.
Hatimaye Bunge limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa yenye jumla ya shilingi trilioni 6.02 ambapo shilingi trilioni 4.4 kwa ajili ya matumizi ya ofisi na zaidi ya trilioni 1.6 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Akijibu hoja mbalimbali za wabunge kabla ya kupitishwa kwa bajeti hiyo, naibu waziri wa nchi ofisi ya rais Tamisemi Mhe. Seleman Jafo ametoa wito kwa halmashauri zote nchni kuhakikisha kuanzi Julai Mosi mwaka huu halmashauri zote nchni zinatakiwa kukusanya mapato yake kwa mifumo ya kieletroniki ili kuongeza mapato ya serikali.
Kwa upande wake akijibu hoja za baadhi ya wabunge waliotaka kujua ahadi ya serikali ya kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji katika mwaka wa fedha 2016/17 kwa ajili ya maendeleo zimetengwa katika fungu gani la bajeti la wizara ya Tamisemi, waziri wa fedha na mipango Mhe. Dkt Phillip Mpango amesema.
Kwa upande wake akijibu hoja za wabunge walitoka serikali kuleta mswada utakao wezesha mkurugenzi wa Takukuru kufikisha kesi mahakamani bila ya kupata kibali cha mkurugenzi wa mashtaka, mwanasheria mkuu wa serikali amesema sheria iliyopo inatoa fursa kwa mikurugenzi wa Takukuru kufikisha mahakamani baadhi ya kesi bila ya kupata kibali cha mkurugenzi wa mashtaka.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni