Zaidi ya wafanyabiashara 2961 walioko maeneo yasiyo rasimi kuondolewa Kariakoo.
'
Uongozi wa manispaa ya Ilala unatarajia kuendesha oparesheni kubwa ya kuwaondoa zaidi ya wafanyabiashara 2961 waliko katika maeneo mbalimbali yasiyo rasimi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuwapeleka katika maeneo ambayo yametengwa.
Uamuzi huo wa manispaa ya Ilala umetangazwa na mkurugenzi wa manispaa hiyo Bw. Isaya Mngurumi ambapo amesema miongoni mwa masoko watakayopaswa kwenda huko ni pamoja na soko la Kigogo Freshi, soko la Tabata, na eneo lililomkabala na gereza la Ukonga.
Miongoni mwa opareshezi zilizoshindwa kufanikiwa ni ile iliyotangazwa mapema mwishoni mwa mwaka 2015, yakuwaondosha machinga Kariakoo na kuwapeleka Jangwani ambapo anasema kwasasa wamejipanga vema kwa kushirikiana na jeshi la polisi pamoja na mgambo wa manispaa na kwamba hakuna machinga yeyote atakaye salia katika maeneo yasiyo rasmi.
Hata hivyo wafanyabiashara wanasema tamko hilo itawawia vigumu kulitekeleza kwani biashara zao zinafana palipo na idadi kubwa ya wananchi.
Source:ITV
Maoni
Chapisha Maoni