MWADUI YAPELEKA JANGWANI KOMBE LA VPL..


Kocha wa Mwadui FC ametangaza kuikabidhi rasmi Yanga kombe la VPL baada ya kuichapa Simba kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jioni ya leo.
Simba watajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga walizozipata kwenye mchezo kabla ya kubanwa na kutunguliwa bao katika dakika za lala salama.
Jamal Mnyate ndiye shujaa kwa upande wa Mwadui kutokana na kupachika bao pekee katika mchezo huo na kuihakikishia timu ya Mwadui ushindi wa ugenini.
Mambo muhimu kufahamu
  • Mchezo wa kwanza Mwadui ikiwa mwenyeji wa Simba kwenye uwanja wa CCM Kambarage timu hizi zilitoka sare ya kufungana bao 1-1, ilikuwa December 26, 2015.
  • Mara ya mwisho Simba kushinda kwenye mchezo wa ligi ilikuwa March 19, 2016 ilipoifunga Coastal Union magoli 2-0 kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
  • Simba haijapata ushindi tangu ilipofungwa na Coastal Union kwa magoli 2-1 kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup.
  • Hii ni mara ya tatu Simba inacheza dhidi ya Mwadu, mechi mbili zikiwa ni za ligi mechi moja ya kirafiki ya kujipima nguvu iliyochezwa kabla ya kuanza kwa msimu huu wa ligi na timu hizo kutoka suluhu (0-0)
  • Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza mechi 27 za ligi huku ikiwa imebakiza michezo mitatu ili ligi kumalizka.
  • Mwadui imebakiza mechi mbili kuhitimisha michezo yake ya ligi, ipo katika nafasi ya sita ikiwa na jumla ya pointi 40 baada ya kushinda mchezo dhidi ya Simba.
  • Katika mechi 27 ambazo Simba imecheza, imepata ushindi kwenye mechi 18, imetoka sare mara 4 na kupoteza michezo 5 huku ikiwa imefunga magoli 43 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 15 hivyo inatofauti ya magoli 28
  • Mwadui imejipatia ushindi mechi 11, sare 7 na kupoteza mechi 10 kati ya mechi 28 ilizocheza. Imefunga magoli 28 na kufungwa magoli 26, inaofauti ya magoli mawili ya kufunga na kufungwa.



Source:Shaffihdauda




































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..