Muziki wa Snura wapigwa marufuku..

Snura na albamu yake chura iliopigwa marufuku Tanzania
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku wimbo na kanda ya video ya muziki kwa jina chura wa msanii Snura Mushi kuchezwa katika vyombo mbalimbali vya habari hadi pale msanii huyo atakapoufanyia marekebisho wimbo huo.
Vilevile Serikali imesitisha maonyesho yote ya hadhara ya mwanamuziki huyo hadi pale atakaposajili kazi zake katika baraza la taifa la sanaa BASATA.
Hatua hiyo inafuatia maudhui ya utengenezwaji wa video hiyo ambayo serikali inasema inakiuka maadili ya raia wa Tanzania.
Serikali imesema kuwa kazi ya mwanamuziki huyo inadhalilisha tasnia ya muziki nchini Tanzania.



Source:BBC













































































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..