Trump asema ataangalia upya mahusiano ya Marekani na China..

Mgombea urais wa Republican, Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa chama chake huko Burlingame, California, April 29, 2016.
Mgombea urais wa Republican, Donald Trump akizungumza kwenye mkutano wa chama chake huko Burlingame, California, April 29, 2016.

Mgombea anayewani uteuzi wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, amesema Marekani haiwezi “kuendelea kukubali China kubaka nchi yetu” wakati wa kampeni yake akiahidi kupanga upya mahusiano ya Marekani na dunia.
Trump amerejea usemi wake kwamba nakisi ya biashara kati ya nchi hizo mbili inasababishwa na China kuidhulumu Marekani na kusema uwelevu wake utaondoa ukosefu wa uwiano.
"Tutalibadili hili" alisema Trump jana Jumapili wakati wa mkutano wa kampeni katika jimbo la Indiana. "Tuna nguvu nyingi sana na China."
Uchaguzi wa kesho Jumanne katika jimbo la Indiana unaonekana ni muhimu ili kuwa mgombea wa chama cha Republikan mwezi Novemba. Kura kadhaa za maoni zinaonyesha Trump akiongoza dhidi ya Seneta Cruz ikiwa ni pamoja na kura ya maoni ya NBC iliyotolewa jana Jumapili inaonyesha Trump akiongoza kwa asilimia 15.



Source:VOA












































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..