Njaa yanyemelea vijiji viwili Kilosa..


Vijiji viwili vya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro huenda vikakumbwa na njaa baada ya mashamba yao kudaiwa kugawiwa kwa wageni.
Vijiji hivyo ni vya Mvua na Gongwe vilivyoko katika Kata na mashamba hayo ya mpunga ambayo yako katika mradi wa skimu ya umwagiliajia, yanafikia ekari 1,320.
Taarifa za uvamizi huo zimeshatolewa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, John Henjewele, alipofanya mkutano wa hadhara na wanavijiji hao.
Wamemwambia mkuu huyo wa wilaya kuwa mradi ulianzishwa kwa  masharti ya kutumiwa na wakazi wanaozunguka eneo hilo, kinyume na hali ilivyo sasa.
Wanavijiji hao wameulaumu uongozi wa umoja wa wakulima wa umwagiliaji (Uwaumvu) ulioamua  kuamua kuyagawa mashamba hayo bila kuwapa taarifa.
Kutokana na tuhuma hizo,  Henjewele ameamua kuuvunja uongozi wa umoja huo na ameagiza kuanzia sasa mradi huo usimamiwe na wataalamu wa kilimo wa wilaya na kijiji, wakiongozwa na ofisa ardhi wa wilaya hiyo.

Source:Mwananchi

























































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..