Majaliwa amwakilisha JPM London.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliondoka jana jioni kwenda London, Uingereza kumwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano wa wakuu wa nchi kujadili mapambano dhidi ya rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika kuanzia kesho.

Majaliwa alisema anakwenda kumwakilisha Rais kwa sababu siku hiyo atakuwa anahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Alisema tukio la Uganda limepewa umuhimu kwa sababu Dk Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa.

Tanzania imealikwa kwenye mkutano huo wa Uingereza ulioandaliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, David Cameron baada ya kufanya vyema katika mapambano dhidi ya rushwa kutokana na juhudi zilizochukuliwa na Serikali.

Alisema mkutano huo unahudhuriwa na wakuu wa nchi 60 zikiwamo “Tanzania na Nigeria ambazo ndizo pekee kutoka Afrika.”

Kwenye safari hiyo, Waziri Mkuu ataongozana na Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki-Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine Mahiga; Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Valentino Mlowola na wataalamu wa masuala ya rushwa na sheria.



Source:Mwananchi













































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..