Mwizi wa pikipiki afia hospitali akitibiwa..


Chiza Dastan (31), anayesadikiwa kuwa mwizi wa pikipiki amefariki dunia Hospitali Wilaya ya Bukombe akipewa matibabu baada ya kupigwa na nyundo kichwani wakati akijaribu kupora pikipiki.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema tukio hilo lilitokea Mei 20 saa 4.00 usiku nje ya Baa ya Geen View, Kata ya Katente wilayani hapa.
Mwabulambo alisema Chiza ambaye ni mkazi wa Kilimahewa, alifariki dunia wakati akitibiwa baada ya kujaribu kupora pikipiki ya Nassoro Tadeo aliyemkodi kutoka mjini Ushirombo kwenda kwenye baa hiyo. Alisema wakiwa nje ya baa, ghafla mhalifu alianza kuongea na watu wasiojulikana kwenye simu, mwendesha bodaboda alishtuka na kutaka kuondoka.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Mahona Kaji alisema majeruhi alipokelewa akiwa na hali mbaya kutokana na kupondwa na kitu kizito kichwani, fuvu la kichwa lilionekana limepasuka. Dk Kaji alisema walijitahidi kuokoa maisha yake lakini ikashindikana.


Source:Mwananchi


























































































































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..