Vyombo vya habari vyatakiwa kuwa na ushirikiano mzuri katika utemndaji wa kazi zao..
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi MH, Hamadi Rashid Mohammed amevitaka vyombo vya habari nchini kuwa na mashirikiano mazuri katika utendaji wao wa kazi ili jamii iweze kufaidika kwa kupata habari .
Amesema uhuru wa vyombo vya habari ni jambo la msingi katika utawala bora hivyo amevitaka vyombo vifanye kazi zake vizuri kwa mujibu wa sheria ili viweze kuelimisha jamii kwa ufanisi.
Hayo ameyasema leo huko katika ukumbi wa nyerere ulioko ocean view Kilimani wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Amesema vyombo vya habari , mwandishi wa habari ni muhimu sana kinachotegemewa katika jamii ambapo kwa kuoitia huko jamii inaweza kupata matukio yote yanayotokea duniani aidha kwa kusikia kuona au kusikia matukio yanayotokea duniani.
Hamadi amesema vyombo vya habari, mwandishi wa habari na vina wajibu mkubwa ukizingatia uwanja mpana wa habari kufikisha kwa jamii katika kufichua maovu na kutangaza mambo mazuri kwa njia ya kuelimisha kuburudisha na pia kuhamasisha.
Pia ameelezea kwamba serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga katika kuwawekea mazingira mazuri kwa vyombo vya habari na waandishi katika utendaji wao wa kazi za kila siku kwani jamii kila siku inapenda kupata habari.
Alisisitiza kuwepo mashirikiano mazuri kwa vyombo vya habari kutaweza kuiletea jamii faraja na kuwa na hamu kubwa ya kuzufuatilia habari zao na hasa zikitolewa kwa wakati.
Amesema iwapo kutakuwa na mashirikiano mazuri kwenye vyombo vya habari vitaweza kujiletea heshima katika umoja wenu na jamii pia.
Sambamba na hayo alitoa nasaha kwa vyombo vya habari katika utendaji wake kwa kutekeleza vyema majukumu yake kwani maadili ya habari ni muongozo katika kazi zetu.
“Waandishi wa habari ni watu muhimu sana na tunafanya nao kazi vizuri hivyo tunawaomba wazitumie kalamu zao vizuri kwani wakizitumia vibaya amani inaweza kutoweka, na wakizitumia vizuri amani itadumu kwani amani ni kitu muhimu “, alisisitiza.
Waziri alivishukuru na kuvipongeza vyombo vya habari katika kipindi chote cha wakati wa uchaguzi kwa kuandika habari za ufasaha bila kuandika habari za uchochezi na kuweza kumalizika zoezi zima la uchaguzi kwa salama .
Kongamano hili limetayarishwa na Zanzibar press club ambapo ziliwasilishwa mada mbili ambapo wajibu wa mamlaka za umma kustawisha uhuru wa vyombo vya habari kama nyezo ya kukuza utawala bora na uwajibikaji nchini.
Na mada nyengine wajibu na majukumu ya taasisi za kihabari kulinda kutetea na kuhifadhi uhuru wa vyombo vya habari na wanahabari Zanzibar ambapo ujumbe wa mwaka huu UPATIKANAJI WA HABARI NA UHURU WA KIMSINGI
imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Source:ZanziNews
Maoni
Chapisha Maoni