Chama cha ACT Wazalendo kimeahidi kuifanya Tanzania kuwa nchi inayojitegemea..



Chama cha ACT Wazalendo kimeahidi kuifanya Tanzania kuwa nchi inayojitegemea kutokana na matumizi sahihi ya raslimali zilizopo  ikiingia madarakani mara baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu. 

Akihutubia wananchi katika mikutano ya hadhara katika majimbo ya Bukombe na Mbogwe mkoani Geita wakati akimuombea kura mgombea urais wa ACT Wazalendo Anna Mghwira, mgombea mwenza wa chama hicho Hamad Yusuf amesema watanzania hivi sasa wapo tayari kwa mabadiliko ya kweli yatakayoongozwa na chama hicho. 
 
Kampeni meneja wa chama hicho Danson Ulotu amewataka watanzaniakujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura huku wagombea wa nafasi za ubunge katika majimbo ya Bukombe na Mbogwe mkoani Geita wakieleza kuwa wananchi katika maeneo hayo wanakabiliwa na matatizo makubwa ya afya, elimu na miundombinu.








SOURCE:ITV




















































Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

USAJILI WENYE MANUFAA EPL HADI SASA..