Mchezo wa gofu kuponza wafuasi wa chama tawala Uchina...
Chama cha Kikomunisti Uchina kina wanachama 88 milioni.
Chama tawala nchini Uchina kimewapiga marufuku wanachama wake wote kujiunga na klabu za mchezo wa gofu.
Agizo hilo la chama cha Communist Party limetolewa kwenye maagizo mapya zaidi kuhusu nidhamu chamani.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Xinhua, chama hicho chenye wanachama 88 milioni pia kimepiga marufuku ulaji sana wa chakula na unywaji pombe pamoja na matumizi mabaya ya mamlaka.
Chama hicho kiliwahi wakati mmoja kuonya viongozi wake wasihudhurie dhifa za kifahari na wasinunue keki kwa kutumia pesa za umma.
Uchina imekuwa ikiendesha kampeni kali ya kupambana na ufisadi tangu 2012.
Sheria hiyo mpya kuhusu mchezo wa gofu inasema wanachama wamepigwa marufuku “kujipatia, kuwa na au kutumia kadi za uanachama za vituo vya kufanyia mazoezi ya viungo yaani gym, klabu, klabu za gofu au kuwa na kadi za wateja au matumizi zinazowawezesha kujiunga na klabu za kipekee”.
Watakaopatikana wakifanya hivyo wanaweza wakapewa onyo au hata kufukuzwa chamani.
SOURCE:Bbc Swahili
Maoni
Chapisha Maoni