Majibu ya Louis van Gaal baada ya kupondwa na Paul Scholes…
Kocha wa klabu ya Manchester United Louis van Gaal ambaye wengi wamekuwa wakihoji juu ya mahusiano yake na wachezaji wa timu yake pamoja na aina ya mbinu anazotumia kuifundisha timu hiyo, October 30 amejibu kauli za kiungo wa zamani wa timu hiyo Paul Scholes ambaye October 29 aliponda mbinu za kocha huyo.
October 30 Louis van Gaal amejibu juu ya kauli ya Scholes ambaye alilenga kukosoa mfumo wa kocha huyo, Scholes alisema kwa sasa mfumo wa Man United sio mzuri na asingeweza kufurahia kucheza kikosi hicho akiwa chini ya Van Gaal. October 30 Louis van Gaal amemjibu Scholes ambaye ni mchezaji wa zamani wa Man United mwenye heshima klabuni hapo.
Paul Scholes
“Hana mamlaka yoyote hivyo anaweza kusema kila kitu kwa ajili ya faida yake au klabu, sitaki kujitetea kwa sababu siwezi kujitetea, nafikiria Scholes kama nguli wa klabu alipaswa kuongea na kocha au rafiki yake Ryan Giggs au Ed Woodward lakini sio kwa njia aliyoichagua kwa sababu atakuwa akilipwa na BBC au SKY, siku zote huwa na kauli ya kidachi fimbo na mawe ndio inaweza kuvunja mifupa lakini sio maneno”>>> Louis van Gaal
SOURCE:Millardayo.com
Maoni
Chapisha Maoni