Tangazo la Twitter kwenye runinga lakanganya...
Wengi walitoa maoni yao kuhusu ubunifu na ucheshi kwenye tangazo hilo.
Tangazo la kwanza la mtandao wa kijamii wa Twitter kwenye runinga limewaacha baadhi ya watazamaji wa televisheni Marekani wakiwa wamekanganyikiwa.
Tangazo hilo la kupigia debe mtandao huo lilikuwa na jumbe kutoka kwenye Twitter kuhusu mchezo wa besiboli, na lilionyeshwa wakati wa kupeperushwa moja kwa moja kwa mechi ya kumaliza msimu wa ligi ya World Series.
Hata hivyo, maandishi yalipita upesi na baadhi ya watazamaji walikimbia mtandaoni kueleza kushangazwa kwao na tangazo hilo.
Mmoja wa watumiaji wa Twitter aliandika kwenye mtandao huo wa kijamii: “Tangazo hilo lilikuwa mbaya sana. Hata siamini linaweza kumvutia mtu kutumia mtandao huo au hata akaona thamani kamwe.”
Mwanablogu John Gruber alisema tangazo hilo halieleweki na akaongeza: “Kuna mtu anafaa kufutwa kazi.”
Baadhi hata hivyo walifurahishwa na tangazo hilo, na mmoja wao aliandina: “Tangazo hilo la Twitter ni bomba.”
Mtandao wa Twitter umekuwa ukitatizika kuvutia watumiaji wapya, jambo ambalo wengi wanasema linatokana na ugumu wa kubadilika wa mtandao huo.
Nembo ya mtandao wa kijamii wa Twitter.
“Mimi ni shabiki wa besiboli na nimekuwa kwenye Twitter 2007, na kusema kweli nilitatizika kuuelewa,” mjasiriamali mmoja wa kidijitali George Nimeh, anayehudumu katika Chuo cha Uongozi wa Kibunifu cha Berlin anasema.
“Siwezi kufikiria jinsi mtu ambaye hajawahi kuisikia Twitter anaweza kudhani mtadhani mtandao huo ni nini (kwa kufuata tangazo hilo).”
Bw Nimeh aliongeza kuwa ingawa takwimu za wafuasi wa Twitter zilionyesha waliongezeka sana mwaka baada ya mwaka, ukuaji huo ulishuka hadi asilimia 20 kufikia mapema mwaka 2015.
SOURCE:BBC
Maoni
Chapisha Maoni