Wananchi watakiwa kujiepusha na vitendo vya uvunjifu amani wakati wa uchaguzi...
Vyombo vya dola, wananchi pamoja na vyama vya siasa watakiwa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani ya nchi ikiwemo upendeleo, matusi au lugha za kudhalilisha utu na kusababisha taifa kuingia katika machafuko katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Ikiwa imebaki siku moja tu ya jumamosi ili watanzania kupiga kura, mtandao wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi hapa nchini, wamesema kwa kipindi kilichobaki ni vyema wagombea wote kunadi sera zao na kujiepusha na matumizi ya lugha za kudhalilishaji utu pamoja na vitisho kwani kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha vitendo vya uvunjifu wa amani huku takukuru nao wakikumbushwa kusimama katika nafasi yao.
Mwenyekiti wa mtandao huo wa asasi za kiraia wa kuangalia chaguzi nchini Bi Martina Kabisama ametoa wito kwa wananchi wote kutumia fursa ya Octoba 25 kupiga kura huku wakazi wa jiji la Dar es Salaam nao wakionyesha kuamasika kuhusu upigaji kura.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni