Jeshi la Polisi Ruvuma limefanya tamasha la michezo kwa ajili ya kulinda amani wakati wa kupiga kura.
Zikiwa zimesalia siku mbili za wananchi kupiga kura kuwachagua Rais,Wabunge na Madiwani jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanya tamasha la michezo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kulinda amani wakati wa kupiga kura jumapili Oktoba 25 mwaka huu.
Tamasha hilo ambalo limefanyika uwanja wa majimaji mjini Songea limeshudiwa na mamia ya wananchi na michezo iliyofanyika ni kukimbiza kuku,kuvuta kamba kati ya raia na polisi ambapo timu ya polisi imeshinda,mchezo wa baiskeli na mchezo wa mpira wa miguu kati ya timu ya polisi na mletele ambapo timu ya mletele imeshinda goli mbili kwa moja na hapa kamanda wa Polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Mihayo Msikhela anaeleza maudhui ya tamasha hilo.
Wananchi na wanamichezo wameeleza umuhimu wa tamasha hilo ambapo zawadi mbalimba lizimetolewa kwa washindi.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni