Walinda amani wa umoja mataifa waachiwa huru Sudan kusini..
Walinda amani wa Umoja Mataifa nchini Sudan Kusini.
Stephane Dujarric, mseamaji wa umoja mataifa, alisema walinda amani hao walikamatwa Jumatatu wakati wakisindikiza meli ya Umoja wa Mataifa ilokuwa imebeba mafuta ya petroli kwenye mto Nile.
Walinda Amani 20 wa Umoja wa Mataifa waliokamatwa na waasi huko Sudan Kusini wameachiwa huru kwa mujibu wa afisa wa Umoja wa mataifa lakini wakandarasi 12 wa Umoja wa mataifa huko Sudan Kusini wanaendelea kushikiliwa.
Msemaji wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric alisema walinda amani hao walikamatwa Jumatatu wakati wakisindikiza meli ya Umoja wa Mataifa ilokuwa imebeba mafuta ya petroli kwenye mto Nile.
Msafara huo ulikuwa ukisafiri kaskazini mwa mji wa Malakal wakati walipozuiwa na watu zaidi ya 100 wenye silaha wa kundi la wapinzani la SPLA ambalo liliwakamata walinda amani hao , wafanyakazi na meli ya mizigo .
SOURCE:VOA
Maoni
Chapisha Maoni