Maalim Seif ahitimisha mkutano wa kampeni za uchaguzi mkuu Unguja...
Shughuli za kijamii na kibiashara katika mji wa Zanzibar na viunga vyake zimesimama kwa zaidi ya saa tano, kufuatia maelfu ya wakazi wa mji huo kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa kufunga kampeni za mgombea urais wa Zanzibar Mh. Maalim Seif Sharif Hamad zilizofanyika katika uwanja wa Maisara.
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha wananchi –CUF, anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA), Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia maelfu ya wananchi wa Zanzibar, amemsihi rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na rais wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mh. Dk. Ali Mohamed Shein kutenda haki katika uchaguzi huo ili kuepusha vurugu na machafuko.
Mgombea mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema), Mh. Juma Duni Haji amesema kwa mara ya kwanza, Tanzania imepata mgombea urais anayekubali serikali tatu - ambapo kwa muktadha huo Zanzibar itakuwa mamlaka kamili bila kuathiri muungano.
Mjumbe wa baraza kuu la Chadema taifa Janet Fussi, meneja msaidizi wa kampeni za urais –CUF, Mansoor Yusuf Himid pamoja na mzee Hassan Nassoro Moyo wanasema serikali iliyoongozwa na Dk. Ali Mohamed Shein imefifisha kabisa matumaini waliyokuwa nayo wazanzibar kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa na mwafaka wa pamoja.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni