Mahakama ya DSM yaahirisha kesi ya kikatiba kuhusu tafsiri ya mita mia hadi kesho..
Hatimaye mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imesikiliza kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kada wa Chadema anayeiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kwamba wananchi wanatakiwa kukaa mita ngapi baada ya kupiga kura shauri ambalo limekuwa na mvutano mkali wa kisheria na kupelekea shauri hilo kushindwa kutolewa uamuzi wake hadi kesho saa tano asubuhi.
Keshi hiyo ambayo inasikilizwa na jopo na majaji watatu wakiongozwa na jaji Sakieti kihiyo limevuta hisia za watu mbalimbali ambapo akitoa maelezo yake naibu mwanasheria mkuu wa serikali Dk Jackson Tulia amesema shauri hilo linapaswa kutupiliwa mbali kwa sababu sheria iliyotumika ni sheria ya mtu anayeweza kuleta maombi kwa haki ya kikatiba iliyovunjwa.
Akaongeza kuwa upande wa mlalamikaji walipaswa kutumia sheria inayoruhusu sheria za uingereza na siyo waliyotumia awali na hivyo suala hilo linapaswa kutupiliwa mbali.
Mbali na maelezo hayo mwanasheria huyo amesema ibara ya 74 kifungu cha kumi na mbili cha katiba hakiruhusu mahakama yoyote kuchunguza jambo ambalo limekwisha pitishwa na tume ya uchaguzi .
Akaoangeza kuwa mbali na sababu hizo lakini pia malekezo yaliyotolewa na rais Jakaya Kikwete ni maelekezo ya kusisitiza yale yaliyokuwa yameelezwa na tume na hivyo hakuna kosa lolote alilofanya na istoshe maelezo yalitolewa na tume ya uchaguzi yalilenga kuhakisha kuwa uchaguzi unakuwa huru na salama.
Kwa upande wake wakili Peter Kibatala anayemtetea mteja wake Ammy Kibatala amesema maelezo yaliyotolewa na naibu mwanasheria wa serikali hayana mashiko kwa sababu yanalenga kuficha uhuru na uwazi wa watu katika kushiriki katika zoezi la kupigha kura.
Akaongeza kuwa japo sheria zinaeleza mambo mbalimbali ya kufanya wakati wa kupiga kura lakini siyo kweli kuwa kuna uhuru wa kuamua kila jambo bila ya kuzingatia haki na uhuru wawatu hata hivyo mawakili wote baaada ya kuahirishwa kwa shauri hilo walielezea namna linavyokwenda na ukizingatia kuwa lipo mahakamni hapo kwa hati ya dharura.
SOURCE:ITV
Maoni
Chapisha Maoni